
Rubens Mikindo kada wa chama cha UDPS nchini DRC amekutana vijana mjini Goma hii ijumaa tarehe 9 septemba 2022. Ni katika lengo la kutafuta ujenzi wa amani jimboni Kivu ya kaskazini.
Mkutano ni katika lengo kuhamasisha vijana ili ya ujenzi wa amani ya kudumu nchini DRC. Vijana walionyesha kwamba serkali inajukumu katika ujenzi wa amani nchini. Pamoja na hayo, vijana pia wanajukumu katika ujenzi wa amani jimboni Kivu ya kaskazini, anena kada huu Rubens Mikindo.
Katika mazungumzo yao, Rubens Mikindo aliyekuwa wazari wa nishati pia mafuta ya petroli aliomba vijana kutounga mkono wafanya siasa, wakiwatumia katika vitendo haramu, ili ya kuzorotesha usalama jimboni.
Aliomba vijana kuondoka ndani ya kundi za maadui wa amani, Maana wafanya hayo kwa manufaa yao wenyewe, siyo ya vijana.
Akihojiwa kuhusu swala la Bunagana, Rubens Mikindo anena kwamba swala hilo lahusu kila mkongomani. Na anaamini kwamba Raisi Félix Antoine Tshisekedi na serkali yake watajitahidi kutafuta amani.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.