DRC/ Sheria: milioni 65 dola za marekani, kipande moja ya tano kuhusu machafuko waliofanya askari jeshi wa Uganda nchini DRC

Tayari dola milioni 65 za marekani, kipande moja ya tano ya pesa za kulipa DRC, kuhusu vitendo vya ujeuri walivyo vitenda wanajeshi wa Uganda nchini humo zimefikishwa. Ni baada ya uamzi toka korti ya sheria ya kimataifa.

Ndivyo alifahamisha waziri wa sheria nchini DRC Rose Mutombo, wakati wa kikao cha sitini na nane cha mawaziri nchini, iliyofanyika tarehe 9 septemba 2022 mjini Kinshasa.

Kuhusu matokeo ya mkutano iliyosomwa naye mnenaji wa serkali Patrick Muyaya, waziri wa sheria nchini anena kwamba nchi ya Uganda italipa mara tano fidia kwa DRC, katika swala la jeshi la Uganda nchini DRC. Na kwa kila kipande ni milioni 65.

Duru hiyo yaeleza kwamba pesa hizo zimewekwa ndani mfuko wa pekee wa wizara ya sheria, katika Benki ya mahali. Na zitaweza kutumiwa wakati vipande vyote vitaenea, Tangazo hilo laeleza kwamba ni jamaa za wahanga ndizo zitatolewa pesa zenyewe, kulingana na machafuko iliyofanyika na jeshi la Uganda nchini DRC.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire