DRC/ Kinshasa : Vijana mashariki mwa DRC waunga mkono Prezidenti wa chama cha kisiasa UNC, Vital Kamerhe kwa kutafuta amani

Akingojewa mjini Goma hii juma tatu 12 septemba, Prezidenti wa chama cha kisiasa UNC, alipokeya mjini Kinshasa vijana wa eneo la mashariki mwa DRC. Hawa ni wa jimbo za Kivu ya kaskazini, kusini, Maniema na Ituri. Ni katika lengo la kumusindikiza katika ya safari yake kwa kutafuta amani mashariki mwa DRC, na kwenyi kanda la maziwa makuu.

Katika habari zilizotolewa kwa wenzetu , vijana hawa walipeleka kwake Vital Kamerhe mbuzi, maziwa, ndizi, nguo ya mkewe na taa.

Katika mafasiria yao, taa inamaanisha mwangaza. Taa hiyo itasaidia Prezidenti wa UNC kutowa mwangaza ill kuleta amani mashariki mwa DRC, na kunako kanda la maziwa makuu
 » Taa hii itakusaidia kuhusu mwangaza, ili kuleta amani na maendeleo popote ambako giza ingali. Peleka taa hii, ili mwanga ionekane kwenyi ngazi za juu mahariki mwa DRC na kunako kanda la maziwa makuu, » vijana wanena.

Prezidenti wa chama UNC alishukuru kuhusu umoja wa vijana mashariki mwa DRC kiutamaduni. Akiamini kwamba taa hiyo itasaidia ili amani na maendeleo vitande mashariki mwa DRC, na kwenyi kanda la maziwa makuu. Akiambia vijana kwamba wasipojipigania, hakuna atakaye leta suluhu kwa shida zao.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire