Goma: Prezidenti wa chama cha kisiasa UNC Vital Kamerhe anangojewa kwa shamra shamra mjini.

Tangu asubui mapema watu wamoja walikutaniwa kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, wakingojea kufika kwake Prezidenti wa chama UNC Vital Kamerhe. Inje na ndani ya lupango ya uwanja wa ndege, raia wamoja waonekana wakivaa vazi nyekundu.

Bwana Arajabu Amani tuliyemkuta kwenyi uwanja wa ndege aeleza : Mimi nimefika kwenyi uwanja wa ndege tangu saa moja, na sasa ni saa tatu kamili. Ninayo furaha kubwa moyoni mwangu kungojea Prezidenti wangu Vital Kamerhe. Hakuna kitaweza nizuiya kumungoja Prezidenti wa chama UNC chake mheshimiwa Vital Kamerhe. Niko hapa hadi atakapofika ili nimutege sikio, aeleza mwanameba huyu tuliyemhoji kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire