Watu hufariki dunia miongoni mwao Afisa moja wa FARDC kwenyi barabara Mbao Kamango

Magaidi wa ADF wameendesha tena shambulizi dhidi ya askari jeshi wa FARDC hii juma tano tarehe 14 septemba kwenyi barabara Mbao Kamango mjini Béni jimboni Kivu ya kaskazini.

Mnenaji wa operesheni Sokola1 luteni Anthony Mwalushay aliyetowa habari anena kwamba ni watu tano ndio walifariki. Miongoni mwao waasi nne wa ADF na afisi moja kwa jina la kanali Mbonza Lucien wa kitengo cha 3402 yaani régiment kwa kimombo. Huyu alikuwa akitokea Beni na kujielekeza pa Kamango.

Katika mapigano hayo ya ADF na jeshi la taïfa, ADF nne waliuwawa na silaha moja kunyanganywa.

Mnenaji wa Sokola1 aongeza kuwa walinzi wa ofisa huyo aliyeuliwa walienda kujiunga na askari jeshi ambayo waliendelea kufwata adui yaani wanamugambo ADF kwenyi mbuga la kuhifadhi wanyama la virunga.

Duru zanena kwamba ni kila mara ndipo shambulizi laripotiwa kwenyi eneo hilo.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire