Goma: Wafungwa ndani ya jela Munzenze waishi katika hali mbovu

Kutokana na ripoti ya watetezi wamoja wa haki ya binaadam, mjini Goma, hali ya wafungwa kwenyi jela kuu Munzenze ni yenyi kuzorota. Ukosefu wa chakula na mengineo.

Mtetezi wa haki ya binaadam mwanasheria Léopold Bagula alijieleza kwa wenzetu wa Agoragrands, kwamba, ukosefu wa chakula jelani humo inaonekana na mengineo, pamoja na ukiukaji wa haki ya binaadam.

Duru hiyo yaeleza kwamba wafungwa waishi humo kupitia misaada. Mfano wa mashirika za kiutu ambazo zatowa chakula. Na hata makanisa mbali mbali nazo zajitowa kila mara kwa huduma hiyo.

Ijapo sheria kuhusu wafungwa inalazimisha hawa wale mara tatu kwa siku, Ila siyo yafanyika, kutokana na hali iliyomo, anena mtetezi huyo wa haki ya binaadam.

Pamoja na hayo, mtetezi huyo wa haki ya binaadam azungumza pia kuhusu maradhi ndani ya jela hiyo, ambayo yahatarisha pia maisha ya wafungwa. Huyu akiombwa serkali kujihusisha na swala la wafungwa kwa kuwa ni haki yao.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire