Kivu ya kaskazini : Wafanya kazi wawili husika na mambo ya udongo wamesimamishwa kazi naye liwali wa jimbo Constant Ndima Kogba

Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Constant Ndima Kogba amewasimamisha kazi wafanya kazi kazi wawili wa serkali , wakishutumiwa kutumika vibaya. Ni mabwana Nyesa Mabutwa husika na mambo ya udongo kunako mtaa wa Karisimbi. Mwengine ni Bwana Lubala Kalumuna kiongozi ndani ya ofisi moja wilayani Rutshuru.

Kutokana na barua yake liwali wa jimbo ya juma tatu tarehe 19 septemba 2022, Bwana Nyesa ashutumiwa kuuzisha kiwanja ilio tayarishwa kwa ujenzi wa kituo moja cha afya mtaani Karisimbi. Pamoja na hayo, Lubala Kalumuna ashutumiwa naye kupokonya pesa za serkali kiwango cha zaidi milioni mbili franka za Kongo.

Kwa hiyo, liwali wa jimbo achukuwa hatua ya kuwasimamisha kazini kutokana na uongozi mubaya, wakipokonya mali ya uma.

Tufahamishe kwamba ni ma Bwana Buaoho Akilimali na Saleh Seyenga ndio watatumika kwenyi nafasi zao kwa muda hadi mipango mingine itakapochukuliwa.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire