DRC : Walimu wa vyuo vikuu na yunivasti wakijumwika ndani ya muungano REPUICO wanena kuanzishwa mara tena kwa magomo

Katika mkutano mkuu wa alhamisi tarehe 22/ septemba 2022 walimu wa vyuo vikuu na yunivasti wa muungano REPUICO wanena kwamba watasimamisha kazi, kwenyi eneo lote la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Wakiomba serkali kutimiza ahadi yake.

Wakati wa kikao hicho mjini Kinshasa, walimu hawo walazimisha serkali kuheshimu makubaliano ya Bibwa. Ambayo serkali inapashwa kulipa mara pili pesa kwa kununua ma gari za kazi . Pamoja na hayo ,kulipa marupurupu kuhusu kazi za utafwiti kama iliyo ahadi.

Hawa wanena kwamba serkali isipotimiza mambo hayo watabaki nyumbani bila shaka.

Walimu wa REPUICO waomba ngazi za kitaifa na kimataifa kuwa shahidi kuhusu swala hilo. Wakiomba viongozi wa serkali kuchukua jukumu kuhusu vinyume vya mgomo huo, utakaoanza punde si punde.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire