Béni: Kamanda wa polisi mjini humo ameonyesha watu wanne wanashumiwa kuendesha vitendo vya wizi

Kamanda mkuu wa polisi mjini Béni Kahumba Lemba Jean Fabien ameonyesha watu wanne wanaozaniwa wizi wakati mkutano wa askari polisi mjini humo. Ni juma tatu tarehe 26 septemba 2022.

Watu hawo walinaswa nyumbani mwa mfanya kazi moja wa MONUSCO, ambamo walipora vitu vingi vya samani. Ilikuwa usiku wa juma mosi tarehe 24 kuamkia juma pili tarehe 25 septemba 2022.

Duru toka polisi mjini humo zaeleza kwamba kijana mwengine alinaswa akizaniwa vitendo vya wizi. Akitaja wenzake ambao wanakuwa wakiendesha pamoja operesheni hizo haramu.

Mhusika na kesi toka polisi huko Naasson Murata anena kwamba, watu hawa wote watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria wasikilizwe na kujibu kwa makosa yao.

Jambo hilo lawafurahisha wakaazi wamoja mjini Béni jimboni Kivu ya kaskazini.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire