Kivu ya kaskazini : Wakati liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini aomba raia kuendesha kazi zao, shirika la raia lasisitiza kuendelea kwa mgomo hii juma nne tarehe 27 septemba 2022

Uratibu wa shirika la raia jimboni Kivu ya kaskazini kwa ushirikiano na vikundi vya wana harakati wa kiraia wamesema kufaulu kwa mgomo walioianzisha hii juma tatu tarehe 26 septemba 2022, kwenyi eneo lote la jimbo la Kivu ya kaskazini. Wakinena kwamba soko, shule na hata ofisa kadhaa hazikufungua milango.

Upande mwengine liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Constant Ndima Kogba ashukuru raia walio heshimu mwito wake, akiwaomba kuendesha kazi zao.

« Niliamuru vyombo vya usalama kupinga maandamano hayo. Nikiomba raia kuendesha kazi zao. Kwa kuwa hayo yanasababisha mauaji na kuharibu majengo, jambo hatuwezi kukubali. Pia wana harakati hawa hawana vikartasi halali kisheria »,anena liwali wa jimbo.

Uratibu wa shirika la raia pamoja na vikundi vya wana harakati wa kiraia waomba raia kuendesha mgomo hii juma nne tarehe 27 septemba 2022.

Kwa ukumbusho hawa wanaomba serkali kufukuza magaidi M23 pa Bunagana, kuondoshwa kwa uongozi wa kijeshi na hata Monusco kwenyi DRC.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire