Mwanabunge wa taifa Ayobangira Safari anena mbele ya wandishi habari kuwa, Prezidenti wa bunge la taïfa Christophe Mboso ameahidi kufwatilia swala la wanabunge wamoja wenyi kushotwa vidole, kuunga mkono maadui wanaosababisha usalama mdogo mashariki mwa DRC.
« Prezidenti wa bunge la taïfa Christophe Mboso amesema kwamba wanabunge wamoja wako nyuma ya maadui wa usalama. Na kwamba ana orotha ya wanabunge hawa. Ila sijuwe kwa nini hakufwatiliya swala hilo. Ijapo hâta vyombo vya usalama vina kuwa na habari kuhusu jambo hilo. Prezidenti wa bunge alinena kwamba ana mamlaka ya kutowa watu hawo kwenyi vyombo vya sheria. Na kwa nini sheria haifwatilie jambo hilo. Ingawa sheria haijihusishe na swala lenyewe, sisi sote mabunge mashariki mwa DRC, tutazaniwa kuwa nyuma ya adui. Ijapo ni jambo lenyi kugusa wamoja kati yetu, » anena mwanabunge huyo mcaguliwa wa Masisi.
« Pamoja na hayo vita huko Bandundu kati ya kabila la Teke na Yaka. Huko ni eneo la kuzaliwa lake Prezidenti wa bunge la taïfa. Tunazani kwamba sheria itafanya kazi yake kutokana na swala hilo. Kama sivyo, vita hivyo vitaweza kutanda kwenyi eneo lote la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Na kukwamisha harakati za uchaguzi ambao tunatarajia. Wanasiasa wamoja wasio jiaminia wajiunga na kundi zenyi kumiliki silaha, ili kukwamisha udemokrasia nchini, » aeleza mwanabunge Ayobangira Safari.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.