Kinshasa : Tahazari imetolewa kwa yule atakaye shambulia watu wenyi umbo la kinyarwanda

Raia mjini Kinshasa watolewa angalisho, kutoshambuliya ama kuwafunga raia wenyi kuwa na umbo la kinyarwanda. Yule atakaye shikwa katika kitendo hicho atapelekwa mbele ya vyombo vya sheria

Katika tangazo lake kamisa mkuu wa polisi mjini Kinshasa kamanda Sylvano Kasongo, anena kwamba , inabidi raia kuepuka jambo hilo, kwa kuzania kuwa kila mwenyi umbo la kinyarwanda ni adui wa DRC.

« Tunatowa mbele tahazari ili watu wasije wakanaswe ndani ya mtego, kwa kushambulia raia wenyi umbo la kinyarwanda. Kila munyarwanda si adui wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo. Maadui wanajulikana vizuri, » asisitiza kamanda mkuu wa polisi mjini Kinshasa Sylvano Kasongo.

Tufahamishe kwamba hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na kufungwa kwa watu wakishakiwa kuwa magaidi wanyarwanda. Hayo yalifanyika hii alhamisi tarehe 30 septemba 2022 mjini Kinshasa.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire