Kivu ya kusini/ Kamanyola: Hali ilikuwa ya heka heka kutokana na kuchomwa kwa askari jeshi moja na raia

Bonde la Ruzizi.

Duru toka bonde la Ruzizi pa Kamanyola jimboni Kivu ya kusini zaeleza kwamba hali ilikuwa ya kutisha hii juma pili tarehe 2 oktoba 2022. Raia wakipinga usalama mdogo eneo hilo.

Kisa ni kwamba mvunja noti moja alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wenyi kumiliki silaha. Wakipeleka hata kiwango kikubwa cha pesa.

Ndipo vijana kuandaa doria wakimnasa askari moja aliyezaniwa kuwa miongoni mwa wenzake wawili ambao walizaniwa kuendesha wizi. Wakati walikuwa mbioni, huyu alianguka ndani ya mfereji. Ndipo raia kumunasa , na kumuchoma kwa rafla.

Baadae mituto ya risasi ilisikika askari wenzake kuonyesha hasira na kutaka kuogopesha raia. Tangu juma tatu asubui raia waliweka vizuizi kwenyi barabara kuelekea Ngomo na pia upande wa mpaka Rwanda na DRC.

Shirika la raia pa Kamanyola lanena kwamba askari hawo ni wapya ndani ya eneo.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire