Rutshuru : Askari jeshi moja na akina mama wauliwa kwa kupigwa risasi, wakikutwa katika kitendo cha ngono

Habari toka wilaya ya Rutshuru zaeleza kwamba askari jeshi moja wa FARDC pamoja na muke wa mwenziwe wamefariki dunia wakipigwa risasi, wakati walikuwa wakifanya unzinzi.

Habari zilizotolewa kwa wenzetu wa le volcan news zaeleza kwamba ajali hiyo ilifanyika pa Mabungo si mbali na senta ya kiwanja wilayani Rutshuru jimboni Kivu ya kaskazini.

Duru zingine toka hapa na pâle ni kwamba ni mume wa mke huyo ndiye azaniwa kumuuwa mkewe pamoja na mwenziwe wa kazi. Duru zaendelea kwamba ni majira ya saa nane usiku ndipo kulisikika milio ya risasi.

« Tulipo jaribu kwenda kwake kiongozi wa kata ili kumpasha habari, tulikuta njiani miili mbili ; moja ni ya akina mama ambaye alipigwa risasi shingoni. Mwili ingine ni yake askari jeshi aliyekutwa ndani ya kitendo cha ngono, alipigwa risasi mguuni na tumboni, » aeleza mkaaji moja toka wilaya ya Rutshuru. Na kwamba askari jeshi aliyeuliwa alikuwa tayari rafiki ya mke wa mwenziwe.

Tufahamishe kwamba miili hiyo ilipelekwa kwenyi hospitali kuu pa Kiwanja tukiwa tu wilayani Rutshuru.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire