Kivu ya kaskazini : Watu kumi wameuliwa na wengine ishirini kupotea, kutokana na magaidi ADF pa Béni.

Watu kumi na moja wamefariki dunia wakiuliwa na wengine ishirini kupotea kutokana na waasi ADF kwenyi kijiji Vido, kwenyi umbali wa kilomita karibuni tano na senta Kainama, mjini Béni jimboni Kivu ya kaskazini

Duru toka shirika la raia zaeleza kwamba miongoni mwa waliouliwa mwapatikana pasta moja wa kanisa la kianglikani. Wengine yapata ishirini wamepotea. Hayo yalifanyika hii juma nne tarehe 4 oktoba 2022 saa za usiku.

.Shirika la raia laomba askari jeshi FARDC pamoja na wale wa UPDF kufanya yote iwezekanayo ili kurudisha usalama eneo hilo. Pamoja na hayo kuandaa msako ili kugundua adui mahali anafichama.

Hali hiyo ilipelekea kazi za kiuchumi na kijamii kuzorota eneo hilo la Beni jimboni Kivu ya kaskazini hii juma nne tarehe 4 oktoba 2022.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire