Goma: Dreva moja ameuliwa kwa kupigwa risasi na askari polisi wakati wa msako

Dreva moja amefariki dunia kwa kupigwa risasi na askari polisi hii juma nne tarehe 12 oktoba 2022. Hayo yalifanyika kwenyi nafasi inayoitwa monument des Rasta kati kati ya mji wa Goma.

Duru zetu zaeleza kwamba mtu huyu alipigwa risasi baada ya ugomvi mkubwa na askari polisi hawo, wenyi kuhusika na kucunguza vikarkasi pamoja na ushuru wa ma gari.

Duru zaongeza kwamba mwili wa Dreva ilipelekwa kwenyi chumba cha wafu kunako hospitali kuu mjini Goma.

Viongozi kadhaa pamoja na wana harakati wa shirika la raia walaumu hali hiyo, wakiomba viongozi wa serkali kukomesha kwanza vita ilioko pa Bunagana pahali pa kujihusisha na misako.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire