Bukavu : Raia wauwa mwizi moja kwenyi kata Nkafu

Raia wenyi hasira kubwa wameuwa mwizi moja kwenyi kata Nkafu mtaani Kadutu mjini Bukavu Kivu ya kusini. Hayo yalifanyika munamo usiku wa juma tano tarehe 11 kuamkia alhamisi tarehe 12 oktoba 2022.

Duru zaeleza kwamba kundi ya wevi hawo ilishambulia nyumba ya Bwana Fidèle Mema mkaaji wa avenue Hôpital général katani Nkafu mtaani humo wa Kadutu.

Walipo taka kujipenya ndani ya nyumba ya mhanga, majirani wakijiunga na jamaa lililoshambuliwa, walikimbiza wevi hawo, wakinasa moja miongoni mwao na kumuondolea maisha.

Duru zaongeza kwamba askari polisi walijitokeza nyuma mno na kujaribu kumpeleka mhanga hima hospitalini, ila alikuwa tayari ameaga dunia.

Shirika la raia la Nkafu laomba wakaaji kujiunga na vyombo vya usalama. Na kwa serkali, kuwapa vifaa walinzi wa usalama ili kufanya kazi yao vilivyo.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire