Hawa walikuwa wakitafuta kuendesha maandamano ya amani, ili kupinga usalama mdogo ambao unatanda jimboni Kivu ya kaskazini, na hata kuvamiwa na waasi wa M23 pa Bunagana. Ni hii juma mosi tarehe 15 oktoba 2022.
Duru zetu toka Béni zaeleza kwamba wana harakati yapata ishirini wamezuwiliwa na askari polisi kunako barabara Joseph Kabila, mbele ya mchana kati mjini Beni, si mbali na hospitali Matanda .
Habari toka hapa na pale zanena kwamba wakati wa maandamano, wana harakati hawa walikuwa wakiimba nyimbo za huzuni. Hiyo ni kutokana na machafuko wanayoitenda pia waasi ADF mjini Beni na penginepo. Kwenyi mabango walioipeleka imeandika: Ikomeshwe mauaji ya kimbari. Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo siyo nafasi ya machinjo ya raia.
Hawa walijikuta kuzuwiliwa na askari polisi, wakitupwa ndani ya gari hadi kwenyi kituo cha polisi mjini humo.
Issa Lubiri.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.