Jeshi la taifa FARDC limenasa hii juma pili tarehe 16 oktoba 2022, wanamugambo wawili mayi mayi. Ni kwenyi kijiji Kisalala kunako barabara Béni Butembo, kaskazini mwa mji. Ilikuwa wakati wa shambulizi la kundi mayi mayi dhidi ya ngome ya jeshi la taifa FARDC.
Mnenaji wa operesheni Sokola 1 Antony Mwalushay anena kwenyi vyombo vya habari kwamba hata silaha ya vita ilishikwa na jeshi la taifa FARDC.
« Ngome ya jeshi la taifa FARDC lipatikanalo kwenyi kijiji Kisalala lilishambuliwa hii juma pili tarehe 16 oktoba na waasi maji maji. Wakati wa kujibu kwa shambulizi, askari Jeshi FARDC walinasa wanamugambo wawili wa kundi mayi mayi, na kunyanganya hata silaha ya vita. Waasi maji maji hawo wakijifananisha na raia, duru zaeleza.
Tufahamishe kwamba shambulizi lingine la waasi maji maji dhidi ya ngome ya jeshi la taifa halikufaulu usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa tarehe 14 oktoba pa Munzambayi, mtaani Vulamba mjini Beni.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.