Kivu ya kaskazini : Ma afisa wa FARDC wamefunguliwa kesi wakishutumiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwa Bunagana mikononi mwa waasi wa M23

Ma afisa wawili ambao walianzisha operesheni mwezi julai pa Bunagana wamefunguliwa kesi na mahakama ya kijeshi. Hawa washutumiwa kuwa chanzo cha kuanguka kwa Bunagana mikononi mwa waasi wa M23 tangu mwezi julai uliopita.

Afisa hawo ni Lobo Kamaghanda na Diadia wa diada . Wanashutumiwa kukimbia adui , ukiukaji wa kanuni na kupora mali ya uma.

Duru toka sheria ya kijeshi zaeleza kwamba ma afisa hawo wanaweza kuhukumiwa kifungo cha kifo.

Kutokana na hali yao ya afya, watetezi wao wameomba watolewe uhuru kwa muda, ila mahakama imetupilia mbali ombi kama na lile.

Tufahamishe kwamba ni tangu mwezi julai 2022, ndipo Bunagana mpakani na nchi ya Uganda ilianguka mikononi mwa waasi wa M23, hadi sasa.

Kipindi cha tatu cha kesi hiyo kinapangwa kuendeshwa tarehe 19 novemba mwaka tunao kwenyi mahakama ya kijeshi jimboni Kivu ya kaskazini, ambako ma afisa hawo wamefungwa.

Chumba cha wandishi.

.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire