DRC : Itabidi kila mwanachuo awe na kompyuta yake, na ndio shurti nyipya ya kujiorodhesha kwenyi vyuo vikuu na yunivasti

Waziri husika na vyuo vikuu pia yunivasti Muhindo Nzangi Butondo amenena kwamba shurti nyipya ya kujiandikisha shuleni, ni kwamba mwanachuo anunuwe kompyuta yake binafsi.

Waziri Muhindo Nzangi alitamka kwenyi média Bosolo na politique mjini Kinshasa mji mkuu wa DRC. Ni hii juma tatu tarehe 17 oktoba 2022.

« Mwanachuo anapashwa nunuwa kompyuta yake binafsi, ambayo ni shurti kwa kujiorodhesha kwenyi yunivasti na vyuo vikuu. Haiwezekane mwanachuo ashindwe kutumia kompyuta. Tutaiga mfano wa Uganda, Pwani la pembe na kadhalika. Kompyuta hiyo itanunuliwa kwa dola za marekani 200. Mwanachuo akilipa nusu nusu, yaani dola 15 kwa mwezi, » aeleza waziri Muhindo Nzangi.

Huyu aongeza kwamba vyuo vikuu na yunivasti kadhaa vimeanza kutumia Wi Fi kwa bure, ila wanachuo wengi hawakufahamu namna ya kutumia Wi Fi hivyo. Ndipo ilibidi kuweka alama inayorahisisha kuingia ndani ya mtandao ya utafwiti peke.

Wazazi wengi wasiojiweza nchini DRC wasema kushindwa malipo ya Kompyuta, kwa kuwa wengi miongoni mwao hawana kazi, Ijapo wanahitaji watoto wao wajifunze teknolojia nyipya.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire