Kivu ya kusini : Kuondoka kwa Monusco wilayani Shabunda kumeleta hofu ndani ya raia wa huko

Ni tangu juma tatu tarehe 17 oktoba 2022 ndipo Monusco wilayani Shabunda ilifahamisha kuondoka moja kwa moja eneo hilo. Shabunda ambayo yapatikana kwenyi umbali wa kilomita 300 na mji wa Bukavu, jimboni Kivu ya kusini.

Habari zahakikishwa pia na serkali ya jimbo la Kivu ya kusini. Ni vikosi vya jeshi wa Indonezia ndio wataanza ondoka moja kwa moja. Jambo ambalo halikufurahisha wakaaji wa huko.

Hawa wakinena kwamba Monusco anawasaidia kwa kazi za usalama na maendeleo.

 » Tunajuta kuhusu kuondoka kwa Monusco. Yeye ametusaidia kwa kutuletea habari za hapa na pale. Habari ambazo zaangazia askari Jeshi FARDC, ili kwendesha kazi yao vizuri. Kuhusu usalama, hakuna shida yoyote ile. Shida moja ni wevi wenyi kupatikana barabaranl kwa kunyanyasa, » aeleza administreta wa wilaya ya Shabunda Benjamin Feruzi kwenyi Redio Okapi.

Duru zaongeza kwamba raia wa Shabunda walipokea bomba ya maji toka Monusco tarehe 26 septemba iliopita. Bomba iliyozinduliwa na administreta wa wilaya hiyo.

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire