Kivu ya kaskazini : Jeshi la taifa FARDC lapigana kwa bidii ili kutowa Bunagana mikononi mwa waasi M23

Askari jeshi FARDC wanahakikisha kwamba wamegunduwa njama za adui, wakiteka nyara wamoja miongoni mwa waasi M23.

Duru toka wilaya ya Rutshuru zaeleza kwamba, tangu asubui ya juma pili, ndipo jeshi la taifa lilionyesha juhudi kwa kuwagonga waasi wa M23, hadi kwenyi umbali wa kilomita 15 na Bunagana, eneo la Kabindi.

Kujumwisha nguvu kwa jeshi la taifa FARDC, ndio ilizusha mara tena mapigano makubwa kati ya waasi wa M23 na jeshi la taifa FARDC eneo la Bweza kwenyi kijiji Bushandala . Ila kimya yaripotiwa kwenyi barabara Jomba Kabindi , eneo ambalo jeshi la taifa FARDC linazibiti.

Mara tena, raia wamehama maskani yao tangu asubui ya juma pili, wakati wa mituto ya silaha nzito nzito. Ni siku inne mfululizo tangu mapigano yarudilie mara tena kati ya waasi wa M23 na jeshi la taifa FARDC wilayani Rutshuru.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire