Bukavu : Shirika nyipya la raia NDSCI latowa malalamiko kuhusu kupokonywa kwa kiwanja ya shule Bwindi

Shirika nyipya la raia NDSCI jimboni Kivu ya kusini latowa kauli kuhusu kutaka kupokonya kiwanja cha shule Bwindi. Shule ambalo ni la kanisa 5ème CELPA. Viongozi wa shule wakiomba shirika nyipya la raia kujihusisha.

Habari zilizo tumwa kwenyi la ronde info, zikisahiniwa naye msemaji wa shirika hilo Wilfried Habamungu, shirika nyipya la raia, lenyi kutetea haki ya binaadam, laangazia kwamba kipande moja cha kiwanja hicho, kimezaniwa kupokonywa na watu wenyi nia mbaya. upande wa Kalengera na Itudu katani Mulambula, mtaani Bagira.

Shirika nyipya la raia NDSCI laomba viongozi kwa kila tabaka, kufika kwenyi nafasi wenyewe, ili kuweka mpaka kwenyi Kiwanja hicho, ambacho kinaonekana kupokonywa. NDSCI inaomba pia liwali wa jimbo, kukinga Kiwanja hicho, ambamo mwapatikana shule la Bwindi ambalo ni la kanisa ya kiprotestanti. Shule lililo wafunza viongozi walio wengi kwa kila tabaka.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire