Ni hii juma mosi tarehe 5 novemba 2022 ndipo vijana 3325 walijiorodhesha ndani ya jeshi, wakikubali kuitumikia nchi yao Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo. Miongoni mwa vijana hawo, wasichana wakikubali pia mwito.
« Butembo, Béni, Lubero, Kanyabayonga na Kayna ni vijana 2100 walijiorodhesha. Goma ni vijana 808, Walikale ni 65, Masisi ni 325, » alinena kanali Ndakala Faustin husika na orodha kwenyi eneo la 34 la kijeshi.
Orodha imefanyika kutokana na mwito wake Raisi wa DRC Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kwenyi Redio ya taifa Rtnc mjini Kinshasa. Huyu akiomba vijana kuingia jeshini kutokana na hali ya uvamizi kila leo, ya Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo na maadui wa usalama.
Tufahamishe kwamba ni juma tatu tangu kuanzishwa mara tena kwa mapigano kati ya jeshi la taifa FARDC na waasi wa M23 wilayani Rutshuru , wakiungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.