Habari toka wilayani Rutshuru ni kwamba waasi wa M23 wamepora ofisi ya Tume huru ya uchaguzi CENI pa Rutshuru ya kati. Hayo yalifanyika majira ya saa tano za mchana. Askari jeshi wa M23 kujitokeza na kupora ofisi hiyo.
Ofisi ya Tume huru ya uchaguzi CENI ikipatikana mbele ya kituo cha polisi na ofisi ya wilaya hiyo ya Rutshuru.
Aimé Mukanda moja wa watetezi wa haki ya binaadam wilayani Rutshuru anena kwamba askari hawo wa M23 walibomowa milango ya ofisi ya Tume huru ya uchaguzi CENI, na kupora vifaa sawa Kompyuta, pikipiki na vinginevyo.
Viongozi wa asili wilayani Rutshuru walaumu vitendo hivyo, tangu kuwasili kwa waasi wa M23 wilayani Rutshuru. Vitendo kama na hivyo vilifanyika hata Bunagana na askari hawo wa M23, ambako duka ziliporwa ndani mukiwa saruji, mabati na kadhalika.
Habari toka waendesha pikipiki ni kwamba hakuna mtu yeyote kutoka Rutshuru ya kati eneo la M23 na kujielekeza mahali pengine, yaani, Goma, Kanyabayonga, Binza na penginepo. Ila watu kutoka nje ya eneo linalozibitiwa waruhusiwa kuingia ndani.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.