DRC- Rwanda : Wanyarwanda washtuka na ndege ya kivita angani mwa nchi yao

Ndege ya kivita aina SUKHOI-25 ilionekana ikizunguka angani mwa nchi ya Rwanda hii juma tatu tarehe 7 novemba 2022, mbele ya mchana kati . Ndege hiyo ikituwa muda mchache kwenyi uwanja wa ndege pa Rubavu magaribi mwa nchi ya Rwanda, mpakani na Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.

Jambo ambalo nchi ya Rwanda ililaumu vikali, ikisema kwamba hiyo ni ukiukaji wa eneo lake kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo nchi jirani.

Baadae tangazo toka ofisi ya mnenaji wa nchi ya Rwanda laeza kwamba kutokana na hali hiyo, hakuna hatua kijeshi zilizochukuliwa, mbele ndege iondoke na kurudi nchini DRC.

Serkali ya DRC ilihakikisha hali hiyo baadae hii juma tatu tarehe 7 novemba 2022.

Issa Lubiri.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire