Walikale : Kundi mbili zenyi kumiliki silaha zimegongana, vifo vingi vikiripotiwa

Ni hii juma tatu tarehe 7 novemba 2022 ndipo kundi mbili zenyi kushikilia silaha zimepigana mbele ya mchana kati. Hayo yalifanyika pa Bukumbirwa na Rusamambu eneo la Ikobo pa Walikale, jimboni Kivu ya kaskazini

Mwanabunge wa jimbo Prince Kihangi anena kwamba ni watu yapata kumi ndio wamepoteza maisha, katika mapigano hayo pande zote mbili, yaani kundi Nduma Défense of Congo NDC na kundi Front Patriotique pour la paix armée du peuple.

Kundi hizo mbili zenyi kumiliki silaha zikipigania ngome ya jeshi la taifa FARDC, aliyoiacha tarehe 26 oktoba 2022.

Hali iliyopelekea raia kukimbia maskani yao hadi Lubero, wakihofia maisha. Pamoja na vitendo vingine vingi vya ukiukaji wa haki ya binaadam mahali hapo.

Mcaguliwa huyo wa Walikale aomba raia wahudumiwe kiutu, pamoja na hayo kutuma askari Jeshi FARDC kwenyi eneo ili kukomesha mizozo , ijapo vita kati ya waasi wa M23 na jeshi la taifa FARDC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire