Goma: Watu wawili wazaniwa utekaji nyara wameonyeshwa mbele ya wandishi habari

Kamanda mkuu wa polisi mjini Goma, kamisa mkuu Job Alisa ameonyesha hii juma nne tarehe 8 novemba 2022, watu wawili washutumiwa utekaji nyara.

Watu hawa wanashutumiwa utekaji nyara mtoto mvulana wa Bi Miriam UMWALI mkaaji kwenyi kata lac Vert, ni miezi mitano sasa. Miongoni mwa washutumiwa munapatikana binti moja mwenyi umri wa miaka 12. Wakati wa kumusikiliza , huyu alionekana kwamba ni yeye aliweza kurahisisha utekaji nyara kwa bwana Obedi, ili kumunasa mtoto wa Bi Miriam, wakisikilizana kuhusu pesa.

Kamisa mkuu Job Alisa alionyesha wazaniwa utekaji nyara hawa mbele ya wandishi habari kabla wapelekwe kwenyi vyombo vya sheria ili kusikilizwa na kujibu kwa makosa yao. Walikuweko mea wa mji wa Goma, kamisa mkuu Kabeya MAKOSA François , na makamu wake Kamisa mkuu KAPEND KABAND Faustin.

Iliombwa kwa kamanda mkuu wa polisi mjini Goma Job Alisa kupeleka binti huyo mdogo kwenyi mahakama husika na watoto, ili asikilizwe mbele ya muamzi wake.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire