Mpasha habari Sonia Rolley wa Redio ya Ufransa RFI ameshurtishwa kuondoka kwenyi ardhi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo hii juma nne tarehe 8 novemba 2022, bila hata kupeleka vifaa vyake. Sababu ya kufukuzwa kwake haijafahamishwa bado.
Kutokana n’a Redio ya Ufransa RFI iliyotowa habari, mwandishi habari alishurtishwa na Shirika la serkali husika na wahami, kuondoka akiingia ndani ya ndege iliyompeleka Parish kupitia Addis Abeba.
Tukumbushe kwamba mwaka 2017 wakati wa utawala wake Joseph Kabila, mpasha habari Sonia Rolley alifukuzwa Mara tena kwenyi ardhi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, akishutumiwa kutangaza habari za vitendo vya ujeuri pa Kwamwina Nsapu huko Kasaï, jambo halikufurahisha viongozi wa DRC.
Mbele ya hapo mwaka 2016, Radio, viongozi wa DRC walisimamisha matangazo ya Redio ya Ufransa RFI kwenyi ardhi ya Kongo. Wakati huo, Lambert Mende mnenaji wa serkali ya DRC, alishutumu Redio hiyo kutangaza habari za vyama vya upinzani ambazo zilipinga hatua kuhusu usalama, iliyochukuliwa na serkali ya Kongo.
Chumba cha wandishi.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.