IRUMU : Watu kumi na wawili wauliwa na watu wasio julikana kwenyi kijiji Masome karibu na Komanda

Habari toka Irumu zaeleza kwamba watu kumi na wawili wauliwa na watu wasio julikana kwenyi kijiji Masome, eneo la Bandiamusu kwenyi barabara Komanda Bunia. Machafuko hayo yalifanyika saa tisa za asubui, watu wakilala.

Shirika la raia pa Irumu laeza kwamba miongoni mwa watu waliouliwa, moja wao alifariki hospitalini. Na kwamba waliotenda kitendo hicho, siyo waasi ADF, ila ni jambazi wengine, maana waasi ADF wanatambulika vizuri na raia.

Duru zingine zenyi kuaminika zahakikisha habari hiyo. Watetezi wa haki za binaadam wa mahali waomba vyombo vya usalama, kujihusisha kinaganaga na jambo hilo, lenyi kutowa raia machozi kila leo.

Duru hizo zahakikisha kwamba tangu kuweko kwa uongozi wa kijeshi, jimboni Ituri, jambazi hujifananisha na waasi ADF, wakitenda vitendo vya kinyama dhidi ya raia.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire