Kivu ya kaskazini : Mea wa mji wa Goma  ahudumia wahanga wa vita

Ni hii alhamisi tarehe 17novemba 2022, ndipo mea wa mji François Kabeya Makosa amehudumia wahanga wa vita kati ya askari Jeshi FARDC na waasi wa M23. Hawa wakitokea wilaya za Rutshuru na Nyiragongo, walitolewa mavazi na viato.

Msaada huo ulitolewa na wakaaji wa mji wa Goma wenyi moyo mwema pamoja n’a ofisi ya meya yemyewe.

« Tuliona muhimu kuhudumia wahami wa vita ambao walikimbia makwao bila kitu. Sisi sawa wanadaam tuliona mhimu kuwatoleya msaada huu kidogo, tukiwaomba wasizarau. Tunaomba watu wengine kufanya hivyo  » anena mea wa mji Kamisa mkuu François Kabeya Makosa.

Upande wa wahami, prezidenti wao Théo Masekura ashukuru kwa msaada huo, akitowa hitaji zingine mbele ya mea yaani ukosefu wa dawa, maji, chakula na vyoo.

Viongozi wa Kinogo eneo la Munigi pamoja na Shirika moja la mahali walikusudiya kuhudumia watoto wanao achiliwa, kwa kuwatoleya uji kila asubui.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire