Kiongozi husika na ulinzi wa mazingira Emmanuel Demerode ashutumiwa kuhudumia kimakao na vinginevyo waasi wa M23, wanaosababisha usalama mdogo jimboni Kivu ya kaskazini.
Huyu ashutumiwa na waziri husika na elimu kwenyi yunivasti Muhindo Nzangi Butondo kwenyi radio Top Congo mjini Kinshasa.
« Ni muda wa kupanza sauti kuhusu ujanja wake kiongozi wa shirika husika na ulinzi wa mazingira Emmanuel Demerode, anayekaa pa Rumangabo, akiwahudumia waasi wa M23 », aeleza waziri Muhindo Nzangi.
Bwana Demerode ashutumiwa kuhudumia waasi hawo kwa mafuta ya petroli na vinginevyo.
« Tuwafahamishe kwamba huyu alikutana na waasi wa M23 pa Matebe, wakikubaliana kwamba waasi watachunga bwawa la moto wa umeme la Matebe. Akiwapa mafuta ya petroli yenyi samani ya dola elfu 20 za marekani. Waasi wa M23 watumia pia gari za shirika ICCN kwa kazi zao, » anena waziri.
Muhindo Nzangi Butondo aomba waziri mkuu makamu pamoja na yule husika na mazingira Eva Bazaiba, kufukuza kazini Emmanuel Demerode, na kusisitisha makubaliano kati shirika lake na serkali ya DRC.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.