Bukavu : Hali ni ya heka heka tangu asubui ya hii juma tano

Hali iliokekana ya vuta ni kuvute hii juma tano tarehe 23 novemba mjini Bukavu. Chanzo ni kibarua kilicho andikwa na wabunge kadhaa kutaka kumuondoa madarakani liwali wa jimbo Théo Ngwabidge Kasi.

Wakaaji wamoja walianza kuchoma gurudumu barabaranl, vizuizi kuwekwa na jumba la ofisi ya bunge kuzingirwa. Akishutumiwa katika jambo hilo Modeste Bahati Lukwebo, prezidenti wa seneti nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. Huyu azaniwa kuwashawishi wabunge hawo, kwa kuwapa kiwango cha pesa yapata elfu mia 300 dola za marekani.

Duru zetu hunena kwamba raia wachukizwa na jambo hilo lenyi kukwamisha maendeleo ya jimbo la Kivu ya kusini kila leo. Wakiomba raisi wa nchi Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kujihusisha ndani ya swala, kwa azibu maadui wanaokwamisha usalama wa jimbo.

Tukumbushe kwamba tangu liwali wa jimbo achukuwe madaraka ‘ni kibarua cha inne sasa, kutaka kumuondoa madarakani, jambo lenyi kuleta vurugu kila mara mjini Bukavu.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire