Goma: Mwanabunge wa taifa Hubert Furuguta aahidi kupiganisha kuhusu amani ya nchi yake hadi mwisho

Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Mwanabunge wa taifa Hubert Furuguta anena kuja nyumbani ili kuishi shida pamoja na raia wa jimbo, kutokana na usalama mdogo inayowakumba.

« Nakuja kubadili fikra na raia, ili kuelewa mambo wazi. Nakuja pongeza raia na askari jeshi, kubaki kuipenda nchi, wakibaki kwenyi msimamo, wakibaki shujaa. Siyo muda tena ya kuacha vita kwa wafanya siasa, Kwa viongozi, Kwa askari jeshi peke. Vita dhidi ya shambulizi, tukifwata historia ya DRC, historia mashariki mwa nchi hiyo , »aeleza Hubert Furuguta.

« Mwanabunge huyu kujiswali kuhusu shambulizi walizo zipata mababu zetu , na kwa nini kuendelea kushambuliwa tukibaki kimya.  » Sasa nakuja kushiriki kwenyi mazungumzo, nikivaa bendera la taïfa, alama ya mapendo na kijitowa ajili ya nchi yangu. Nikiomba wakongomani kuipenda nchi yao, kukinga udongo wao. Navaa pia bendera ya chama changu cha kisiasa. Ni alama kwamba Prezidenti wa chama anabaki mwaminifu kwa kuipenda nchi yake, kwa kijitowa ajili ya nchi yake, akiheshimu matamshi yake. Nami nitabaki mwaminifu », asisitiza Hubert Furuguta Mwanabunge wa taifa.

Huyu aongeza kwamba watu wengi huzani kwamba wakongomani wachukiya nchi yao, na ndio maana wawaonyesha zarau.  » Ni muda sasa il kuwaonyesha kwamba twapenda DRC nchi yetu. Anayependa mali yake huikinga hadi kumwanga damu » anena Mwanabunge Furuguta. Akisema kutokubali ahadi zozote, matamshi yoyote mazuri yasiyo towa matunda, n’a kwamba ni muda sasa kwa viongozi kuacha hotuba zisizofaa, wakiheshimu ahadi.

Juvénal Murhula

 

 

 

 

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire