Hali ilifanana kuwa shwari hii juma pili tarehe 3 julai kunako uwanja wa mapambano kati ya waasi wa M23 na jeshi la taïfa FARDC. Hata hivyo Shirika la raia wilayani Rutshuru lalaumu hali ya kiutu kutokana n’a kuongezeka kwa idadi ya wahami toka eneo za vita.
Shirika la raia wilayani humo laongeza kwamba wahami hao wahitaji huduma ya haraka kwani hawana makao na chakula.
Kanisa la kikatolika laomba Papa wa Roma kujihusisha ndani ya diplomasia ya ujirani bora ili kutekeleza amani Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Kardinali Fridolin Ambongo alifahamisha hayo wakati wa kusoma misa kuhusu amani n’a mariziliano hii juma pili mbele ya jumba la taïfa Palais du peuple kwa kimombo. Misa ilisomwa naye katibu wa nchi ya Vatican.
Tukumbushe kwamba swala kuhusu wahami wilaya ya Rutshuru, wakihofia maisha liligusiwa naye Profesa Daktari Joseph Kitaganya. Mwalimu huyo wa yunivasti aliomba raïa wa DRC kupokea ndugu wakongomani wenyi kuishi hali ya mateso. Akiomba serkali kufanya yote iwezekanayo ili usalama urudi pa Rutshuru. Kwani serkali ina jukumu la kulinda raia na mali yao.
Huyu alisisitiza pia kuhusu kauli moja kwa wakongomani ili kumushinda adui anaye kwamisha maendeleo ya nchi.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.