Masisi : Watu saba kufariki dunia n’a wengine wengi kujeruhiwa Katia shambulizi la jambazi wenyi kumiliki silaha pa Kashuga

Watu saba miongoni mwao wanaume nne na akina mama tatu waliuliwa na wengine wengi kujeruhiwa , na jambazi wenyi kumiliki silaha pa Kashuga, usultani wa Bashali Mokoto, wilayani Masisi, Kivu ya kaskazini. Shambulizi lilifanyika ndani ya Kempi moja ya wahami.

Duru za mahali zaeleza kwamba jambazi hawo hawakujulikana, Ila jeshi la taïfa FARDC lilijitokeza bila kufaulu kuwa nasa.

Bahati Théophile moja wa viongozi wa mahali alaumu kisa hicho mara tena , akiomba uchaguzi ufanyike ili kugunduwa matenda maovu na kuwapeleka mbele ya vyombo vya sheria, ili watolewa azabu.

Huyu aomba raia kutowa mapema wahalifu hawo, na kwa askari polisi kufanya kazi yao, Kwa kulinda raia na mali yao.

Tufahamishe kwamba shambulizi hilo lilifanyika baada ya shambulizi lingine lilijitokeza kunakuwa miezi kadhaa ndani ya kempi jirani ,na kusababisha vifo na majeraha.

Juvénal Murhula.

 

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire