Ituri: Maafa ni mengi watu kuuliwa na vifaa kuharibika katika shambulizi la wanamugambo ADF pa Mambasa

Duru toka wilayani Mambasa zanena kwamba magaidi ADF walijiingiza ndani ya kijiji Makala, eneo la madini pa Lolwa wilayani Mambasa jimboni Ituri. Hayo yalifanyika munamo usiku juma tatu kuamkia juma nne tarehe 6 disemba 2022.

Duru hunena kwamba watu wawili waliuliwa kwa silaha za asili, gari, nyumba kuchomwa moto, watu wengine kutekwa nyara, na kadhalika.

Duru toka polisi pa Mambasa zahakikisha habari, na kwamba askari Jeshi FARDC ndiyo wanazibiti eneo kwa sasa. Na kuongeza kwamba uchuguzi unaendeshwa, ili kufahamu matokeo kamili ya shambulizi hilo.

Tufahamishe kwamba shambulizi ni kila leo wilayani Mambasa jimboni Ituri. Shambulizi lingine lilifanyika wilayani humo hapa karibuni. Wakati akina mama moja na kijana mvulana waliweza kuuliwa na wanamugambo ADF.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire