Kivu ya kaskazini : Vijana wawili wafariki dunia kwa kufyatuliwa risasi

Vijana wawili wafariki dunia kwa kufyatuliwa risasi pa Buhene wilayani Nyiragongo kando ya mji wa Goma. Hayo yalifanyika usiku wa juma nne tarehe 6 disemba 2022, majira ya saa tatu usiku, eneo hilo la jimbo la Kivu ya kaskazini.

Prezidenti wa shirika Jeunes visionnaires du Nord Kivu Hodari Muhave anena kwamba baada ya kutenda machafuko, watenda maovu walinyatuka na kwenda mahali pasipo julikana.

Vijana wawili walifariki dunia wakifyatuliwa risasi na watu wasio julikana , wakitembea kwa pikipiki. Baada ya hapo kunyatuka na kwenda zao, mahali pasipo julikana, anena Prezidenti huyu wa shirika Jeunes visionnaires du Nord Kivu Bwana Hodari Muhave.

Bwana Muhave anaomba viongozi wa jimbo kufanya yote iwezekanayo kwa kulinda raia na mali yao. Huyu anaomba pia viongozi kuongeza idadi ya askari Jeshi eneo hilo, ili kufikia usalama wa kudumu.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire