Rutshuru : Monusco imetuma timu la wachunguzi ili kujionea jisi hali iliyoko eneo za kishishe ambako mauaji ya kimbari ilifanyika

Mauaji ya kimbari iliyofanyika pa Kishishe wilayani Rutshuru imefanya ulimwengu mzima kutazama upande wa mashariki mwa DRC. Ikiwa ni vitendo vya ujeuri na ukiukaji wa haki ya binaadam.

Kwa hiyo ofisi ya Umoja wa kimataifa husika na haki ya binaadam pamoja na Monusco wametuma timu la wataalam , ili kuchunguza hali iliyoko pa Kishishe. Huko raia zaidi ya 272 walifariki dunia. Ni katika mapigano kati ya waasi wa M23 na wanamugambo Mai mai.

Timu lilikwenda huko juma nne tarehe 7 disemba 2022. Ni katika lengo kuchunguza hali iliyoko na namna mambo yalifanyika. Ilikuwa pia fursa ya kuzungumza na viongozi wa mahali na washuhuda, ili kutowa mwanga kamili kuhusu watu walifariki dunia.

Vikosi vya Monusco vimeahidi kukinga raia ambao wanakubali kukimbilia ndani ya kempi yao pa Rwindi. Hata kama wengi miongoni mwao wamekimbilia kwenyi eneo ambazo zazaniwa kuwa na usalama.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire