RDC : Muindaji moja auwa mtoto wake akimufananisha na nyama huko Kasaï ya kati

Mwindaji moja amemuuwa mtoto wake akitumia mkuki, silaha anayoitumia kwa kuinda nyama. Hayo yalifanyika usiku wa juma mosi kuamkia juma pili kwenyi kijiji Kabue sekta ya Musuasua kwenyi umbali wa kilomita 70 na Kazumba, mji kuu wa wilaya yenyi kuitwa kwa hiyo.

Duru za mahali zaeleza kwamba Muindaji alisema kufananisha nyama na mwanae, na ndipo kumchoma mkuki alipokuwa akifanya kazi yake. Duru zaongeza kwamba ajali ni chungu tele katika sekta ya uindaji pa Kasaï ya kati siku hizi.

Walinzi wa usalama wameahidi kufanya uchunguzi ili kujuwa sababu ya ajali hiyo. Ambayo imepelekea huzuni kwa wakaaji wote wapatikanao vijijini.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire