
Tume huru ya uchuguzi CENI imehakikisha kuanza kwa operesheni ya Orotha ya wachaguzi kwa mwaka wa 2023 nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Operesheni ilianza hii juma mosi tarehe 24 disemba 2022 kwenyi eneo mhimu zilizochaguliwa, mfano wa Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Kwa siku ya kwanza, raia walikuwa wenyi furaha kubwa, kwa kupokea haraka kadi za wachaguzi, ambazo ni vitambulisho kwao sawa wanainchi.
Orotha ya wachaguzi ni alama ya kuhakikisha kufanyika kwa uchuguzi tarehe 20 disemba 2022 nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Ikiwa pia mwito kwa wakongomani kwenda kujiorodhesha, ili waweze kujibu kwa siku kuu hiyo.
Tazama mpango wa Tume huru ya uchaguzi munamo siku za usoni:
Tarehe 24 disemba 2022 : mwanzo wa orotha ya wachaguzi nchini DRC
Tarehe 26 machi; kupokea vikartasi vya wakandideti wanabunge wa taifa.
Tarehe 3 agosti 2023: kupokea vikartasi vya wakandideti wanabunge wa jimbo
Tarehe 1 septemba 2023: kupokea vikartasi vya wakandideti kwenyi uraisi.
Tarehe 20 disemba 2023: Uchaguzi nchini DRC kwa jumla.
Tarehe 10 januari 2024 ; kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi kwa jumla
Tarehe 20 januari 2024; kula kiapo kwake raisi mpya wa nchi
Tarehe 12 machi 2024; kushimikwa kwa maliwali wa majimbo
Tarehe 26 machi 2024; kushimikwa kwa ofisi ya uongozi ya bunge la taifa
Tarehe 24 februari 2024; kushimikwa kwa wana seneti nchini.
Tarehe 30 machi 2024; Uchaguzi wa shauri la mji pamoja na viongozi wa mitaa
Tarehe 20 mei 2024; kushimikwa rasmi kwa ofisi ya shauri la mji
Tarehe 27 mei 2024; kuchaguliwa kwa mea wa mji na makamu wao
Tarehe 11 julai 2024; , Uchaguzi wa washauri wa sekta na wale wa usultani.
Tarehe 17 septemba 2024; kuchaguliwa kwa viongozi wa sekta na makamu wao.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.