DRC : Imepokea vifaa vya vita kutoka nchi ya Uturuki

Ni hii ijumaa tarehe 6 januari 2023, ndipo Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Imepokea vifaa vya vita, ili kugongana na waasi wa M23 na wengine wanaoendelea kukwamisha usalama mashariki mwa nchi hiyo.

Ni liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini mwanajeshi jenerali luteni Constant Ndima Kogba ndiye alipokea vifaa hivyo kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma.

Mjumbe wa Uturuki Tayyip Erdogan, amesema kwamba msaada ni alama ya uhusiano kati ya nchi ya Uturuki na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kwa niaba yake Raisi wa DRC na serkali yote nzima, Constant Ndima ameshukuru serkali ya Uturuki kwa msaada huo, ambao umefika wakati inayofaa.

Tufahamishe kwamba msaada huwo umefika siku chache baada ya kuruhusu DRC kununua vifaa vya vita, wakati nchi hiyo ilikuwa imekataliwa  tangu  siku nyingi na Shauri la usalama la umoja wa kimataifa.

Issa Lubiri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire