Goma: Waziri wa kilimo nchini DRC Désiré Birihanze yupo ziarani mwa kazi mjini Goma

Waziri wa kilimo nchini DRC Désiré Birihanze amewasili hii juma nne tarehe 10 januari 2023 mjini Goma. Anakuja kuanzisha majengo ya jumba la ofisi ya widhara ya kilimo jimboni Kivu ya kaskazini. Pamoja na hayo kuzindiwa jengo kubwa ambayo ni gala la kuweka mazao ya kilimo humo tu jimboni.

Akihotubia raia kwenyi wa uwanja wa shule la msinji Byahi mjini Goma, waziri wa kilimo alisema kuwa anakuja na ujumbe wa shukrani wake Raisi Félix Antoine Tshisekedi ajili ya raia wa Kivu ya kaskazini. Hawa wakimuunga mkono ili kupiganisha vita vinavyotokana na nchi ya Rwanda kupitia magaidi wa M23.

Waziri wa kilimo Désiré Birihanze aongeza kwamba DRC itaendelea kufanya yote iwezekanayo ili askari jeshi wapate vifaa na kushinda vita dhidi ya Rwanda.

Waziri alitowa mwito kwa raia kujiorodhesha haraka iwezekanayo ili kupata kadi ya uraia yaani carte d’identité, na kushiriki kwenyi uchaguzi mwaka hui Akisisitiza kwamba ni kupitia Raisi wa taifa, ndipo mara tena wakongomani watapata kadi ya uraia ama carte d’identité.

Wahami wenyi kupatikana ndani ya kempi wataorodheshwa pale pale, kwa kungojea orotha itakayo fanyika baadae kwa raia waliobaki kwenyi vijiji vyao. Ingawa vita haitakoma mbele ya muda wa uchaguzi.

Ijapo waziri wa kilimo kufika ajili ya kuanzisha majengo ya ofisi ya kilimo jimboni, na kuzindiwa jumba ambayo ni gala ya kuweka chakula zaidi ya tani ma milioni ,Désiré Birihanze aliahidi kukutana na raia siku nzima, kuzungumza kuhusu hali ya maisha jimboni na nchni DRC.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire