Kivu ya kaskazini : Watu kumi wameuliwa na thelasini na tisa kujeruhiwa ndani ya kanisa moja ya CEPAC pa Lubiriha Kasindi

Watu kumi wamepoteza maisha na thelasini na tisa kujeruhiwa wakati wa ibada ya ubatizo ndani ya kanisa moja la shirika 8 ème CEPAC pa Lubiriha Kasindi wilayani Beni.

Ikizaniwa kuwa ni magaidi ADF ndio wametenda jambo hilo. Ila mnenaji wa jeshi la DRC pa mahali Antony Mwalushay anena kwamba, moja akishakiwa kuwa miongoni mwa watenda maovu hawo tayari amenaswa. Akiongeza kwamba matokeo hiyo ni kwa muda,

Duru zetu huhakikisha kwamba ni watu kumi waliofariki dunia, na thelasini na tisa kujeruhiwa, wakati wa ibada ya juma pili tarehe 15 januari 2023. Na kuongeza kwamba uchunguzi unafanyika ili kufahamu ni akina nani waliofanya machafuko hayo.

Serkali ya DRC inaendelea kulaumu hali hiyo, Pamoja na hayo Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo atowa mkono wa pole kwa jamaa zilizokumbwa na msiba. Akiahidi pia kwamba uchunguzi utafanyika ili kujuwa wahusika na kuwaazibu kulingana na matendo yao.

Tufahamishe kwamba liwali wa jimbo Constant Ndima apatikana kwa sasa mjini Beni ili ya kujionea hali iliyoko. Huyu amechukuwa hatua ya kuhudumia jamaa zilizokumbwa na msiba kwa mazishi na hata watu waliojeruhiwa kwa matibabu.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire