RDC : Fortunat Biselele mshauri binafsi wake Raisi Félix Antoine Tshisekedi afukuzwa ndani ya ofisi yake Raisi

Akishakiwa uhusiano kati ya nchi ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo mshauri binafsi wake Raisi Félix Antoine Tshisekedi ameondoshwa ndani ya ofisi yake Raisi.

Vile vile Raisi amewaweka kando memba wamoja wa ofisi yake ambao wameonyesha ujanja kazini, na kushukuru wote walioendesha kazi zao vizuri kwenyi ofisi.

Fortunat Biselele alikuwa ameshotwa vidole uhusiano mubaya kati ya nchi ya Rwanda na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Huyu akishutumiwa kutumika kwa siri, hadi kupelekea waasi wa M23 kuteka maeneo karibuni zote wilayani Rutshuru.

Duru zetu kutoka Kinshasa zahakikisha kwamba mshauri binafsi wake Raisi Félix Antoine Tshisekedi alikuwa akiwindwa na shirika la upelelezi, akishotwa kidole katika uhusiano mchafu na Rwanda. Bwana Kahumbu Mandungu Bula ndiye amemugombowa Fortunat Biselele.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire