Kivu ya kaskazini : Kiongozi mwanajeshi wa wilaya ya Beni Ehuta Omeonga Charles aponea chupu chupu mitego ya magaidi

Habari toka wilaya ya Beni ni kwamba Kiongozi mwanajeshi wa wilaya ya Beni ameponea chupu chupu mitego ya magaidi alipokuwa ziarani mwa kazi. Huyu alikuwa katika uchaguzi wa watu waliopatwa na majeraha, ili kuwapeleka kwenyi matibabu. Hawa walishambuliwa na magaidi ndani ya kanisa moja 8ème CEPAC wakati wa ibada pa Kasindi.

Aliponea chupu chupu kwa msaada wa shirika la ujasusi, ambalo lili vuruga mpango wa magaidi kwa kutofaulu.

« Ninashukuru shirika la ujasusi ambalo limeniokowa. Nilikuwa nikiandaa mpango wa kupeleka wahanga wa majeraha kwenyi matibabu. Ambao walishambuliwa ndani ya kanisa moja 8ème CEPAC, wakati wa ibada ya mahubiri, » anena Administreta huyu wa wilaya ya Béni.

Kiongozi wa wilaya ya Beni Ehuta Charles aongeza kwamba alipata habari toka vyombo vya usalama, kwamba adui alikuwa akimuinda ili auwawe. Na kwamba habari ilipojulikana kwa njia ya simu, adui alinyatuka zake.

Ehuta Omeonga Charles aomba viongozi wa mahali kuwa makini kwani adui yupo kando. Akiwaomba kutokusanyika kwa vikundi, kanisani na hata sokoni, kwani wakati wa kukimbia jeshi la FARDC, adui hushambuliya hata vikundi vya watu.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire