DRC : Inakataa mazungumzo yoyote mara tena na nchi ya Rwanda ( Waziri Muhindo Nzangi Butombo)

Kwa sasa senta ya Kitshanga haina shambulizi yoyote ile. Hizo ni mbinu za Kaghame kuchokoza kila leo DRC. Mwafahamu kwamba yeye hataki amani nchini Kongo, ila amekwisha gonga ukuta. Siyo tena wakati wa zamani wakukimbilia nchini Rwanda ajili ya mazungumzo. Wameomba kuwe na mazungumzo, ila Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi amekataa akisema ya kale yamepita.

Haya ni matamshi yake waziri husika na yunivasti nchini DRC Muhindo Nzangi Butombo. Huyu akijielekeza mjini Kisangani ambako ataanzisha rasmi shule ya mafunzo ya kijeshi kwa wanachuo.

Muhindo Nzangi aongeza kwamba DRC imeweza kusahini makubaliano mjini Nairobi na ya huko Loanda. Mazungumzo hayo ililenga waasi wa M23 waondeke haraka kwenyi ngome walizozibiti.

« Tulipata muda yote ya kujitayarisha. Nawahakikishia kwamba mambo yatabadilika hapa karibuni. Hatutakaa meza moja tena na nchi ya Rwanda. Wametaka moto iwake na ni hivyo. » anena waziri.

Akiongeza kwamba mbinu zote za kusaka amani zitatumiwa. Hata kuingia katika makubaliano ya shirika East Africa. Na kwamba hiyo ni utashi mwema kwa DRC ambayo imeonekana kuchoka.

Waziri Muhindo Nzangi alijaribu kujibu kwa swala lenyi kuelekea wahami wenyi kupatikana ndani ya kempi pa Kanyaruchinya, ambao maisha inaendelea kuzorota.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire