Kivu ya kaskazini : Mji wa Goma unakumbwa na shida ya maji tangu juma kadhaa

Akihojiwa na waandishi habari mjini Goma, mwana sheria Je t’aime Hangi aonyesha shida ya ukosefu wa maji safi mjini Goma, tangu siku nyingi. Akiomba viongozi husika kujitahidi, kwani hali hiyo ina hatarisha maisha ya raia.

Mwana sheria Hangi ashangaa kuona hali yaendelea ijapo mji wa Goma unapatikana bega kwa bega na ziwa Kivu, nafasi ya karibu ya kutosha maji.

Sherti viongozi husika wajitokeza kwa kutafuta suluhu ya kudumu.

« Ni huzuni kuona hali hii inadumu mjini Goma. Ni zaidi ya wiki sasa mirija ya maji ni yenyi kukauka. Ijapo kuwepo pembeni kwa ziwa Kivu. Hali hii ina hatarisha maisha ya raia kutokana usalama mdogo mjini. Wasichana nawo hubakwa na watenda maovu », anena Mwana sheria je t’aime Hangi, ambaye pia ni msemaji makamu wa chama cha kisiasa UDPS Kivu ya kaskazini. Akikumbusha mara tena Kiongozi wa shirika Regideso jimboni kuchunguza kwa makini swala hilo. Nakuomba shirika la utowaji umeme SNEL » kutumika bega kwa bega na shirika Regideso, ambalo haliweza faulu katika kazi pasipo mkono wa shirika SNEL

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire