Kivu ya kaskazini : Muungano SVK unaalika raia kwenda kwenyi orodha ili kutayarisha uchaguzi

Tunakuja ili kuomba raia wajiorodhesha kwa kujitayarisha kwenyi uchaguzi. Kwani wanabunge wamoja hawakutumika kama inavyo stahili bungeni. Inabidi wapate fundisho. Hatuwezi baki mjini Kinshasa ijapo raia waendelea kuteswa humu jimboni. Tutakutanana tukiwa kamati jimboni ya shirika SVK, ili ya kupanga kazi. Tunakuja kutimiza mapashwa yetu kama wanainchi wanao upendo kwa nchi yao. Tutaandaa vipindi kwenyi radio na televisheni za mahali. Na mwishowe tutaomba raia wajielekeze kwenyi orodha ya uchaguzi tarehe 16 februari, ambayo itakoma tarehe 17 machi 2023.

Mratibu wa Muungano SVK jimboni Kivu ya kaskazini Matata Kahusi anena hayo kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, hii juma pili tarehe 5 februari akitoka mji mkuu Kinshasa kuhusu ziara ya kazi.

Akihojiwa kuhusu kipi cha mhimu kati ya kutekeleza usalama mashariki mwa DRC na kufanya uchaguzi nchini, mratibu ahakikisha kuwa mambo yote mawili ni mhimu. Akiangazia kwamba Raisi wa taifa na wanainchi wengi wanapiganisha usiku na mcana, ili kurejesha usalama mashariki mwa DRC. Bwana Matata Kahusi aongeza kwamba inabidi uchaguzi ufanyike tarehe 20 disemba 2023 kulingana na katiba ya nchi.

Huyu afahamisha kwamba chama UNC chake Vital Kamerhe kinaendelea kuunga mkono Raisi wa taifa Félix Antoine Tshilombo katika kazi zake. Na kwamba chama hicho kinaendelea kuwa ndani ya Muungano wa kisiasa Union sacrée.

Akizungumzia pia kuhusu mambo ya kidiplomasia, ambayo Raisi wa taifa anaendelea kujihusisha, ajili tu ya kutafuta amani nchini. Akisaidiwa naye moja wa vinara ndani ya siasa ya Kongo Vital Kamerhe.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire